Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo waiva

NA FREDRICK MAHAVA

MAKABIDHIANO ya mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo iliyopo mkoani Rukwa yalifanyika hivi karibuni kati ya Viongozi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga, Mkandarasi Mshauri MD Consultants JV Mhandisi na Mkandarasi wa Ujenzi Works Contractors Ltd.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Elias Essaba (aliyevalia tai) akikabidhi nyaraka muhimu za ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kalambo ikiwemo michoro na mkataba wa ujenzi wa jengo hili kwa Mkandarasi wa Ujenzi kampuni ya Works Contractors Ltd.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Mahakama hiyo ya Wilaya ya Kalambo ambaye ni Kampuni ya Works Contractors Ltd. Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga Bw. Machumu Elias Essaba alimtaka Mkandarasi huyo kuzingatia masharti ya Mkataba ikiwa ni pamoja na kumaliza mradi huo wa ujenzi ndani ya muda uliyoainisha kimkataba.
Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania kutoka Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma Bw. Fabiani Kwagilwa (aliyevalia Kofia) naye alikuwepo wakati wa makabidhiano hayo.

Naye, Mshauri wa ujenzi wa mradi huo kutoka kampuni ya MD Consultants JV Mhandisi alifafanua kuwa, vipengele vyote vya Mkataba wa ujenzi huo vitazingatiwa ipasavyo kwa ushauri na usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kwamba Mkandarasi kutoka kampuni ya Works Contractors Ltd anamaliza kazi hiyo ya ujenzi kwa wakati uliopangwa kwenye mkataba.

Kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Kalambo ujezi huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi nane ambayo ni sawa na siku 240 za kimkataba wakati ambao mkandarasi anapaswa kukabidhi jengo hilo kwa mteja ambaye ni Mahakama ya Tanzania.
Mwakilishi kutoka kwa Mkandarasi Mshauri wa ujenzi wa mradi huo kutoka kampuni ya MD Consultants JV Mhandisi akiwa ameshikilia michoro na ramani za jengo hilo la Mahakama.

Aidha, wakati wa makabidhiano hayo Mtendaji Bw. Essaba aliambatana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Kalambo Mhe. Nickson Temu, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Matai Mhe. Suzan Mkinga, Mhandisi wa Mahakama kutoka Makao Makuu ya Mahakama na Afisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo Bw. Samwel Kamese.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news