Utafiti wabaini faida uboreshaji na usimamizi taka oza Dar

DAR-Utafiti uliofanywa na Dar es Salaam Urban Resilience Programme (DURP), umegundua kuboresha usimamizi wa taka oza kunaleta nafasi nyingi za kupunguza gesi chafu, kupunguza ukubwa wa mafuriko kwenye miji mikubwa na kuboresha udongo kwa ajili ya uzalishaji.
Utafiti huo ulianza wiki ya kwanza ya Januari 2024 na kuhitimishwa Machi 31, 2024 jijini Dar es Salaam, uliotekelezwa chini ya mradi mkubwa wa Green Cities and Infrastructure Programme (GCIP) kutoka Uingereza wenye lengo la kuhimiza ukuaji wa chini wa kaboni kwenye nchi zilizokusudiwa ikiwemo Tanzania.

Hayo yamesemwa Machi 13, 2025 na mwakilishi kutoka DURP Jonathan Williams kwenye warsha iliyowakutanisha wadau wa usafi hapa nchini kwenye Hoteli ya Delta iliyopo jijini Dar es Salaam.

"Usimamizi wa taka oza kutoka kwenye masoko ya mbogamboga na matunda ya Dar es Salaam, ni sehemu muhimu ya mchango wa jiji kwa nchi ya Tanzania katika jitihada za kupunguza hewa chafu, na njia muhimu ya kuboresha jiji kukabiliana na majanga ya hali ya hewa siku za usoni yanayotokana na mabadiliko ya vipindi vya mvua," amesema Williams.

Ameendelea kwa kusema ukuaji wa uchumi unategemea watu na tunajua jiji la Dar es Salaam, ni jiji la tatu linalokuwa kwa kasi zaidi kwenye bara la Afrika hivyo tunahitaji kuwekeza katika watu ili kukuza uchumi wa nchi

Msimamizi Mkuu wa Fedha za tabianchi kutoka DURP, Dkt.Madaka Tumbo amesema utafiti huo ulienda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya njia bora ya kuhifadhi taka kuifanya kuwa mtaji.

"Leo hapa tupo na wadau kujadili namna ya kuthibiti taka mijimi na vijijini ili iwe rahisi kusaidia kwa miradi mingine inayokuja, kama tunavyojua mji unavyotanuka ndio uzalishaji wa taka unavyoongezeka," amesema Dkt.Tumbo.

Huku akiwata wananchi watambue kwa sasa hakuna taka inayopaswa kutupwa kwani kipo kiwanda cha mboji Mabwepande jijini Dar es Salaam kinachukua taka na kuchakata kwa matumizi mbalimbali.

Ofisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Ubungo Ezla Joseph amesema kwenye eneo lake tatizo kubwa ni taka za chakula ambazo ndizo zinazalishwa kwa wingi, hivyo ameona kuna haja ya kuwapa elimu wakazi wa eneo lake ili taka hizo zigeuke kuwa fursa kwao.

"Katika eneo langu la Ubungo lililopo jijini Dar es Salaam wananchi wa eneo hilo asilimia 100 wanazalisha taka zitokanazo na chakula, sasa basi kupitia utafiti huu nitaenda kuwapatia elimu ili wazijue frsa zitokanazo na taka hizo," amesema Joseph.

Dar es Salaam ina masoko ya ukubwa wa kati zaidi ya 20 ya matunda na mbogamboga kwa mji mzima, mengi yana wafanyakazi wa jimla na rejareja, huku idadi ya watu wanaomiliki maduka ya matunda na mbogamboga 2,500.

Utafiti huu umejikita katika masoko makubwa matatu ya matunda na mbogamboga yaliyopo Dar es Salaam, ambapo huzalisha jumla ya tani 55 za taka oza kila siku, masoko hayo ni soko la Ilala, Buguruni na Mabibo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news