VIDEO:Ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa kosa la wizi wa Mita za maji Moshi

KILIMANJARO-Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Moshi Mjini imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela, Shafii Kondo (56) mkazi wa mtaa wa Kiusa kwa kosa la kuiba mita za maji za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Akitoa hukumu hiyo leo Machi 26,2025 Hakimu A.A Mkao amesema anamuhukumu Shafii kwa kosa la kuiba mita tisa zenye thamani ya shilingi laki tisa na kuisababishia mamlaka hasara.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) hivi karibuni ilikabiliwa na changamoto ya baadhi ya wananchi wasio waaminifu kuhujumu miundombinu kwa kuiba mita za maji ambazo zimekua zikisababishia Serikali hasara kubwa.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA Mhandisi Kija Limbe amesema mpaka sasa Mamlaka imepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 22.6 ambazo takribani mita 211 zimeibwa kwa kipindi cha kuanzia Oktoba, 2024 mpaka mwezi wa pili mwaka huu.

Aidha,Mkurugenzi amewataka wananchi hayo ambao sio waaminifu kuacha mara moja kwani kwa sasa Serikali imeweka mbinu mbalimbali za kuwabaini na kuwakamata sambamba na hatua stahiki kuchukuliwa juu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news