KATIBU wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM,CPA Amos Makalla amemtembelea na kumjulia hali Katibu Mwenezi BAWACHA,Bi. Siglada Mligo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Makalla amemtakia Bi.Siglada Mligo matibabu mema na uponyaji wa haraka ili arejee katika majukumu yake.
Aidha,Makalla amesikitishwa na ukimya wa viongozi wa Chadema kutomjulia hali na kuendelea kumbeza Siglada mitandaoni kwani kitendo hicho ni cha kutweza utu.
“Badala ya kufuatilia afya ya kiongozi wa chama chao wamejikita kwenye siasa na kulaumu CCM kuendelea kumsaidia matibabu Bi. Siglada."
Katika hatua nyingine Makalla amemuhakikishia, Bi.Siglada kuwa watampatia matibabu yote muhimu mpaka apone, huu ni utekelezaji wa 4R za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.
Tags
Habari