KILIMANJARO-Kamati ya Siasa Mkoa wa Kilimanjaro imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA).
Mradi huo unaogharimu shilingi milioni 787 unalenga kuhudumia wananchi zaidi ya 10,500 walioko kwenye Kata ya Marangu Mashariki.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Innocent Lugodisha ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji Maji na Usafi wa Mazingira ameihakikishia Serikali mradi huo kukamilika mapema ili wananchi waweze kupata huduma hiyo ya majisafi na salama.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, ndugu Geofrey Mnzava amepongeza na kuishukuru namna Mamlaka hiyo ilivyoweza kutekeleza mradi huo kupitia mapato ya ndani
Ndugu Selemani Mfinanga ambaye ni Mwenezi Mkoa wa Kilimanjaro amefurahishwa na namna usimamizi mzuri wa fedha za Serikali unavyotatua changamoto za wananchi.
Ziara hiyo iliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mhe. Dkt. Charles Kimei ambaye ni Mbunge wa jimbo na viongozi mbalimbali wa Chama, Serikali na Dini.