DAR-Mwinjilisti wa Kimataifa na mfanyabiashara, Alphonce Temba amesema, wanasiasa wanachangia kuharibu uchumi kwa matamko ya kisiasa.
Kutokana na hali hiyo, Temba ameiomba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuunda Tume Huru ambayo itafanya uchunguzi Kariakoo jijini Dar es Salaam ili kuleta majibu zaidi ya malalamiko.
Ameyasema hayo kupitia ujumbe wa video fupi aliyoitoa leo Machi 22,2025 akieleza kuhusu hali ya mivutano inayoendelea Kariakoo.
"Nimesikia kauli ya kikosi kazi na Mheshimiwa Jafo (Dkt.Selemani Jafo) amezungumza kuhusiana na wageni ambao wamekuwa wakitumika na Watanzania wazawa kuficha taarifa.
"Na akazungumzia wako wageni kama 30 ambao walitimuliwa nchini kwa sababu ya udanganyifu huo.
"Lakini, nataka niseme hivi, mara nyingi katika Taifa letu tumekuwa tukipata taarifa za viongozi wakiamua maamuzi ambayo mara nyingine yanaweza yakawa yanaleta gharama kwa sababu wale mawaziri sio wafanyabiashara.
"Jafo sio mfanyabiashara, Kitila (Waziri Prof.Kitila Mkumbo) sio mfanyabiashara alikuwa mwalimu wa Chuo Kikuu na sasa hivi ni waziri, na hiyo nafasi wamekaa mawaziri wengi wakapita, lakini kauli zao wanashindwa kuenenda na wakati wa sasa.
"Hawajawahi kufanya biashara, kwa hiyo wanaingiza maneno yao kuharibu uchumi hasa kuwapendezesha Watanzania.
"Iko hivi, Machinga biashara anayoifanya hasafiri nje, ni hao wafanyabiashara wa China, Wakongo, Waghana, Wanigeria, Wazambia, Wakenya, Waganda wanaokuja kufanya biashara nchini, ndiyo wanaochukua bidhaa zao hizo hizo wanazitembeza mchana na ndiyo wanaokuja kulalamika hao hao, halafu Waziri anakuja kusema na vitu vingine kama hivyo.
"Iko hivi,Mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia nguvu kubwa sana, ni Rais wetu wa kwanza kuja na staili ya kipekee;