VIDEO:Rais Dkt.Samia amefanya zaidi ya matarajio Sekta ya Afya nchini-Hapi

ARUSHA-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, Ally Hapi amesema,Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi kwa juhudi zake katika kuboresha sekta ya afya nchini ndani ya miaka minne ya uongozi wake.
Akizungumza katika Kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka minne madarakani lililofanyika siku ya Jumanne mkoani Arusha, Hapi amesema kuwa jitihada za Rais Samia zimekuwa kielelezo cha kupambana na moja ya maadui wakuu wa taifa ikiwamo maradhi.

"Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba tunao maadui wakubwa watatu: ujinga, umaskini na maradhi. Inawezekana tunao maadui wengi lakini hao ni wakubwa zaidi.

"Rais Samia amefanya kazi kubwa kupambana na adui maradhi kwa kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za afya karibu na maeneo wanayoishi, huku vituo vya afya vikiboreshwa ili kutoa huduma za kisasa," amesema Hapi.

Ameeleza kuwa ndani ya kipindi cha miaka minne, Rais Samia amefanikisha ujenzi wa hospitali za wilaya 129 na vituo vya afya 485 katika kata mbalimbali nchini.

"Katika kipindi chake, kila Halmashauri nchini imepata magari mawili mapya ya kisasa kwa ajili ya huduma za afya. Jirani zetu Wakenya walikuja kujifunza jinsi Rais Samia alivyoleta mageuzi katika sekta ya afya," ameongeza Hapi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news