DODOMA-Kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule na usambazaji wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wenye uhitaji.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule amewapongeza wanawake wa PSSSF kwa mchango huo katika kuboresha mazingira ya elimu hapa nchini na kuwapunguzia adha watoto wa kike kutembea umbali mrefu kufuata shule jambo ambalo linawaweka katika hatari mbalimbali.
"Mmechagua njia nzuri ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo inaacha sura isiyofutika, mngeweza pesa yenu kuishia kula na kufurahi kwa namna yenu lakini mmeamua kutunza kumbukumbu kubwa katika historia ya shule hii;