DODOMA-Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amewataka vijana wa mkoa huo kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa Forum, Mhe. Senyamule alisisitiza kuwa vijana wana jukumu kubwa katika kutokomeza tatizo hili.
Kongamano hilo, lililohudhuriwa na vijana zaidi ya 1,500 kutoka vyuo mbalimbali vya Dodoma, vikiwemo Chuo cha Mipango, CBE, VETA, pamoja na waraibu walio kwenye matibabu, lililenga kutoa elimu na kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)