Vijana wa kike watakiwa fedha wanazopata wazitumie katika uwekezaji

MKURUGENZI wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bi. Ziana Mlawa ametoa rai kwa Vijana wa Kike kuwa fedha wanazopata watumie pia katika kufanya uwekezaji hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi.
Bi. Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akieleza kuhusu nafasi ya Msichana katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini yatafanyika kitaifa mkoani Arusha.

"Pamoja na majukumu yetu tuliyokuwa nayo tukijiwezesha na sisi kwenye uwekezaji itatujengea sana kujiamini kwenye kufanya kazi, ukiwa na uhuru wa kifedha kujiamini kunaongezeka kwenye kazi yako,"amesisitiza Bi. Mlawa.

Amesema Wizara ya Nishati inaitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji” kwa namna mbalimbali ikiwemo suala la usawa kwani katika Wizara watumishi wanawake wapo 82 na wanaume 145 na kueleza kuwa kwa uwiano huo anaamini kauli mbiu hiyo imefanyiwa kazi.

Ameongeza kuwa hata kwa viongozi wa Menejimenti ya Wizara ambayo idadi yao ni 12 wanawake ni watano na wanaume ni 7.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news