Viongozi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Umoja wa Wanasheria Afrika (PALU) na Maafisa Waandamizi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati wa kikao kilichofanyika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa alipomtembelea Wakili Mkuu wa Serikali Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa akielezea namna ofisi yake inavyofanya kazi alipomtembelea Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) Ofisi kwake jijini Dar es Salaam.
Afisa Programu wa Umoja wa Wanasheria Afrika (PALU), Bi. Neema Jaji akielezea lengo la ziara yake walipomtembelea Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) Ofisi kwake jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utetezi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Wakili Paul Kisabo akitoa neno la shukrani baada ya kikao na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) Ofisi kwake jijini Dar es Salaam.