ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali ametoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga na kuwekeza katika hatifungani ya Zanzibar SUKUK kwa ajili ya kupata faida halali.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema kwa kufanya hivyo Serikali itapata fedha za kuendeleza miradi ya maendeleo kwa kuwa na fedha za uhakika na wananchi kupata faida halali.
Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa tayari Serikali imelizingatia wazo la kuwekeza katika Sukuk kwa dola hususani kwa Wazanzibar wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) na sasa wanaweza kuwekeza kwa Dola.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza PBZ kwa kuendelea kutoa huduma bora za kibenki na kuifanya kuwa benki inayoaminika na kutegemewa na wananchi.