Wananchi wafurika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu

ARUSHA-Kufuatia Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotegemea kufanyika Kitaifa jijini Arusha tarehe 8 Machi, 2025 yaliyotanguliwa na maonesho na utoaji wa Elimu kwa Umma katika Viunga vya Uwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini humo, Wananchi wanaotoka katika maeneo ya Mkoa wa Arusha na mikoa jirani wamefurika katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Ni kwa lengo la kujipatia elimu kuhusiana na Masuala mbalimbali yakiwemo ya Menejimenti ya Maafa, uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi, masuala ya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa Serikali pamoja na masuala ya Afua za UKIMWI.
Maeneo mengine ni pamoja na elimu ya mifugo, kilimo na Uvuvi kupitia programu ya Kuendeleza ya kilimo na uvuvi (AFDP) pamoja na Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II).

Watalaam hao wanawake kutoka katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wameonekana wakitoa elimu hiyo kwa makundi mbali mbali ya wanawake wasichana na vijana wa rika tofauti tarehe 07 Machi 2025 na kuendelea.

Maadhimisho hayo yanatanguliwa na Kaulimbiu inayosema "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji".
Aidha katika kuadhimisha kilele ya siku hiyo,Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post