Wanawake Masjala Kuu wanogesha Siku ya Wanawake Duniani

NA ARAPHA RUSHEKE

WAFANYAKAZI Wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu wamesherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kufurahi pamoja katika hafla ya usiku wa Mwanamke iliyofanyika Machi 8, 2025 katika Hoteli ya Midland jijini Dodoma.
Watumishi wanawake wa Mahakama Kuu Masjala Kuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za wanawake zilizofanyika tarehe 08 Machi, 2025 katika Hoteli ya Midland jijini Dodoma.

Watumishi hao wa Masjala Kuu walipata fursa mbalimbali za kubadilishana mawazo pamoja na kufurahi kwa pamoja katika hafla hiyo.

Akizungumza wakati wa kufungua hafla hiyo Mgeni maalumu wa sherehe hiyo ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe.Upendo Madeha alisema kuwa, “tunajivunia kuwa sehemu ya sherehe hii ya kipekee sio kwa utashi wetu bali ni kwa neema za Mwenyezi Mungu ambae ndiye Muumba wa kila kitu, sherehe hii ni maalumu kwa ajili ya wanawake wote Duniani kusherehekea mambo mbalimbali yanayofanywa na wanawake.”
Watumishi wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za Siku ya wanawake iliyofanyika tarehe 08 Machi, 2025 katika Hoteli ya Midland jijini Dodoma.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe.Upendo Madeha akifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri wakati wa sherehe za usiku wa mwanamke zilizofanyika katika Hoteli ya Midland iliyopo jijini Dodoma.
Watumishi wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za wanawake zilizofanyika tarehe 08 Machi, 2025 katika Hoteli ya 'Midland' jijini Dodoma.

Mhe. Madeha alisisitiza upendo mshikamano sehemu za kazi kwani ni jambo muhimu katika maisha yao na linampendeza Mungu na kwamba amefurahi kuona wanawake wa Mahakama Kuu Masjala Kuu wapo pamoja na wanapendana.

Wakiwa katika hafla hiyo wanawake hao walipata elimu ya afya ya mwanamke inayohusu safari ya ukomo wa hedhi iliyotolewa na Mwanaisimu na Mtafiti wa Taifa wa Afya ya Jamii, Bi Aloisia Shemdoe Mhingo.

“Safari hii ya ukomo wa hedhi ni muhimu sana katika kuboresha afya ya Wanawake na jamii kwa ujumla mwanamke akikombolewa jamii imekombolewa ni muhimu sana wanawake kutambua umuhimu wa elimu hii kwani ni walimu bora na walezi kwa watoto,” alisema Bi. Aloisia.
Mwezeshaji wa mada Mwanaisimu na Mtafiti wa Taifa wa Afya ya Jamii (Public Hearth Reseacher ), Bi.Aloisia Shemdoe Mhingo akitoa mada yake wakati wavsherehe za wanawake wa Mahakama Kuu Masjala zilizofanyika kwenye ukumbi wa Midland Hoteli jijini Dodoma.
Keki maalum iliyoandaliwa kwenye hafla ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanywa na watumishi wanawake wa Mahakama Kuu Masjala Kuu.
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hizo wakiwa katika picha ya pamoja.

Aidha, aliwasihi watumishi hao kutumia vitu vya asili ili kuboresha miili yao na afya kwa ujumla.

Katika hafla hiyo watumishi hao walijumuika pamoja na kupata chakula cha usiku kwa pamoja.

Sherehe za siku ya Wanawake Duniani kitaifa zimebeba kaulimbiu isemayo; “Wanawake na Wasichana 2025: “Tuimarishe Haki, Usawa na uwezeshaji.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news