Wanawake STAMICO wahamasisha matumizi ya nishati safi Rafiki Briquettes

DAR-Watumishi Wanawake wa Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) wametumia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
Lengo la hamasa hii ni kuwawezesha wanawake na wasichana kutunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Hayo yamesamwa na Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa STAMICO, Bi Leah Jericho wakati wa maandamano ya kusherehekea siku hii leo tarehe 8 Machi katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salam.
Bi. Leah amesema STAMICO inaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kutoa elimu na kutumiwa na watu wengi zaidi.

Amesema STAMICO imeamua kupeleka nishati ya Rafiki Briquettes kwenye Maadhimisho ya siku hii kitaifa Arusha ili kuonesha kwa vitendo jinsi inavyoweza kutumika kwa namna tofauti kulingana na mahitaji mahsusi.

"Nitoe hamasa kwa wanawake nchini hasa wale wanaotumia nishati chafu za kuni na mkaa unaotokana na miti kuchangamkia nishati hiyo inayopatikana kwa bei nafuu" alisisitiza Bi Leah

Ametumia fursa hiyo kuishukuru menejimenti ya STAMICO kwa kuendelea kutoa nafasi kwa wafanyakazi wanawake kushiriki katika uendeleshaji na usimamizi wa miradi mbalimbali.
Licha ya STAMICO kushiriki kitaifa huko Arusha kwa kuonesha shughuli mbalimbali za Shirika sambamba na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya Rafiki Briquettes, imeshiriki pia katika mikoa ya Dar es Salam, Songwe na Dodoma ambako kuna ofisi zake.

Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ni "Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news