Watumishi wanawake Kanda ya Mbeya mambo yalikuwa hivi

NA MWINGA MPOLI

WATUMISHI Wanawake wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya wamesherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kushiriki hafla ya jioni iliyofanyika Machi 8, 2025 katika ukumbi wa Mahakama Kuu Mbeya hafla iliyoshereheshwa na shughuli mbalimbali zilizokuwa zimeandaliwa.
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (wa kwanza kushoto) Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda Mbeya Mhe. Aziza Temu (wa kwanza kulia) na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi Mavis Miti (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wanawake wakati wa hafla ya kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Watumishi hao walipata fursa ya kupata elimu kutoka kwa Daktari Bingwa wa masuala ya Afya ya Akili na magonjwa ya akili toka Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Mbeya Dkt. Stephano H. Mkakilwac, na pia watumishi hao walipata wasaa wa kubadilishana mawazo, kufurahi pamoja kwa kusakata rumba na michezo mbalimbali iliyokuwa imeandaliwa ukumbini hapo.

Akifungua hafla ya maadhimisho hayo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa aliwapongeza watumishi wanawake hao kwa kushiriki katika hafla hiyo, kwani ni njia mojawapo ya kuwaunganisha watumishi pamoja, na pia alipata wasaa wa kubalishana mawazo juu ya mambo mbalimbali yanayohusu haki, usawa na uwezeshaji wa wanamke katika jamii inayomzunguka.
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (katikati) Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda Mbeya Mhe. Aziza Temu (kulia) na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi Mavis Miti wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akijadili jambo watumishi wanawake wa Mahakama Kuu Kanya ya Mbeya katika hafla hiyo.
Watumishi Wanawake wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa na bashasha nyusoni wakati wa hafla ya kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

“Tukio ili la kutukutanisha ni jambo zuri na niwapongeza wanawake wote kwa kushiriki hafla hii kwani ni njia ya kutuunganisha zaidi. Nitoe rai tudumishe upendo na tufanye kazi kwa bidii tuweze kutimiza lengo Kuu la Mahakama ya Tanzania kutenda haki kwa usawa na kwa wakati kwa jamii tunayoihudumia,” alisema Jaji Nongwa.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili kutoka Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Mbeya Dkt. Stephano Mkakilwa aliwaelimisha watumishi wanawake wa Mahakama juu ya masuala ya kulinda na kutunza afya ya akili na pia dalili za watu wanao athiriwa na afya ya akili katika maeneo ya kazi, na pia watumishi walipata fursa ya kufanya mjadala, kuuliza maswali na kuyatolea ufafanuzi.
Watumishi Wanawake wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa na bashasha nyusoni wakati wa hafla ya kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Miti akikata keki katika hafla hiyo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Rufaa, kanda ya Mbeya Dkt. Stephano Mkakilwa akitoa mada kwa watumishi wanawake Mahakama Kuu Mbeya.

“Mnahitaji muda wa kutosha ili kupumzika mara baada ya muda wa kazi kuisha, ilikuepuka msongo wa mawazo, mshiriki matukio ya pamoja na pia kuepuka matumizi ya vilevi,” alisema Dkt. Mkakilwa.

Aidha, aliwaeleza kuwa wakiweza kuepuka mambo hayo inaweza kusaidia kuepuka mambo yanayoweza kuathiri afya ya akili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news