Watumishi wanawake wa TEA wajitoa kwa jamii

DODOMA-Watumishi wanawake wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo tarehe 7 Machi 2025 wametembelea Kituo cha Kulea Watoto Miuji Nyumba ya Matumaini jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Katika ziara hiyo, wametoa msaada wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo chakula vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.7 kwa ajili ya watoto 65 wanaolelewa kituoni hapo.
Sr. Hellen, mlezi wa kituo, ameishukuru TEA kwa mchango wao, akisema kuwa kituo hicho hutegemea misaada ya wadau ili kuhudumia watoto wake.

Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa TEA, Bi. Alice Lukindo, amesema wanawake wa TEA wameamua kusherehekea siku hii kwa kuleta faraja kwa watoto.
"Wanawake tuna wajibu wa kutunza familia na jamii. Leo tumeamua kugusa maisha ya watoto hawa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news