Wizara ya Afya Tanzania yathibitisha wagonjwa wawili wa homa ya nyani (Mpox)

DODOMA-Mnamo tarehe 7 Machi, 2025 Wizara ya Afya kupitia mifumo yake ya ukusanyaji wataarifa na ufuatiliaji wa magonjwa ilipokea taarifa za uwepo wa wahisiwa wenye dalili zavipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili.
Dalili hizi ziliambatana nahoma, maumivu ya kichwa, vidonda kooni, maumivu ya viungo vya mwili ikiwemo misulina mgongo.

Kati ya wahisiwa hao mmoja ni dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchijirani kwenda Dar es Salaam.

Baada ya kupokea taarifa za wahisiwa, sampuli zilichukuliwa na kupelekwa maabara yaTaifa kwa uchunguzi.

Mnamo tarehe 9 Machi, 2025 uchunguzi wa kimaabara umethibitisha kuwa wahisiwa wawili (2) wana maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox.

Hivyo, hadi kufikia sasa jumla ya wahisiwa wawili (2) wamethibitikakuwa na ugonjwa wa Mpox nchini.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na vituo vyote vya kutoleahuduma za Afya, inaendelea na ufuatiliaji, uchunguzi na utambuzi kubaini kama kunawahisiwa wengine ili waweze kupatiwa huduma stahiki.

Chanzo cha ugonjwa huu ni wanyama jamii ya nyani, ambapo binadamu huweza kuupata kutokana na shughuli zinazoweza kusababisha kugusana na wanyama, majimaji au nyama za wanyama wenye maambukizi.

Aidha, endapo binadamu akipata maambukizi hayo anaweza kumwambukiza mtu mwingine kwa kugusana moja kwa moja.

Kwa taarifa hii, Wizara ya Afya, inawahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kudhibiti ugonjwa huu na hasa kutokana na uzoefu tulionao wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

Serikali inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa katika ngazi zote, upimajiwa watu wanaoingia na kutoka kupitia mipaka ya nchi, kuimarisha utoaji wa elimu ya afya na kuhamasisha jamii ili kuwawezesha wananchi kuchuka hatua za kujikinga.

Kwa kuzingatia kuwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tibamahususi ila mgonjwa anahudumiwa kulingana na dalili alizonazo.

Hivyo, wizara inawasihi na kuwasisitiza wananchi wote kuzingatia na kutekeleza afua za kujikingakama ifuatavyo:

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news