DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Access ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bw. Protase Ishengoma, baada ya kufanya ziara fupi ya kutambulisha shughuli za Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam na kujadiliana kuhusu fursa za ushirikiano kati yake na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Access Bank, Bw. Protase Ishengoma, aliipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii ikiwemo ile ya kimkakati na kuahidi kuwa Benki yake ambayo ina misuli ya kifedha, iko tayari kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo pia kuwa miongoni mwa Taasisi zinazoweza kufanya majukumu ya kuitafutia Serikali fedha za kutekeleza miradi hiyo.