KAMPALA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasili jijini Kampala nchini Uganda jana usiku kushiriki Mkutano wa 50 wa Bodi ya Wadhamini (Governing Council) ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB), utakaofanyika leo tarehe 13 Machi 2025 katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala na kulakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Meja Jenerali Paul Simuli na Viongozi wengine Wakuu wa Benki hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EADB, ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Benard Mono.