MBEYA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) usiku wa kuamkia leo amewasili jijini Mbeya kwa ajili ya kuwa Mgeni Rasmi katika tukio la utiwaji saini wa makubaliano ya Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tunduma hadi Vwawa.
Hafla hiyo itakafanyika katika Viwanja vya Mwakakati-Tunduma mkoani Songwe, kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi leo Machi 20, 2025, mradi unaotarajiwa kuwanufaisha maelfu ya wakazi walioko katika eneo la mradi.
Akiwa na Mwenyeji wake, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, wakati wa futari ya jioni jijini Mbeya,Dkt. Nchemba, alimpongeza Mhe. Aweso kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Miradi ya Maji nchini na kwamba anamheshimisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.