LUANDA-Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amewasili jijini Luanda nchini Angola kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, Rais wa Jamhuri ya Angola.