ROME-Pembezoni mwa Mkutano wa Mpango wa Mattei kwa Afrika na ‘EU Global Gateway’ jijini Roma, Italia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi, Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Tanzania, Mhe. Stergomena Tax aliyekuwa kwenye ziara ya kikazi nchini humo ambapo Tanzania na Italia zimesaini Hati ya Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi.
