Waziri Mchengerwa apiga marufuku malori kupita barabara ya mwendokasi

DAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa tarehe 21 Machi, 2025 amekemea uharibifu wa barabara unaofanywa na Magari Makubwa (Malori) kupita Mwendokasi huku akizitaka Halmashauri na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kufikiri namna bora ya kumaliza foleni ndani ya Dar es Salaam.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya Utiaji Saini wa Zabuni 9 zilizobeba thamani ya Shilingi Bilioni 221.8 zinazojumuisha Barabara zenye urefu wa Kilomita 84.4 zinazotarajiwa kwenda kuboreshwa katika Halmashauri za Dar es Salaam chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP TWO).
Akizungumza wakati wa Hotuba yake Mhe. Mchengerwa amesema Mhe. Rais hatamani kuona foleni, Halmashauri kaeni fikirini namna ya kumaliza foleni ndani ya Jiji hili, mmetoa Kibali Magari kupita Mwendokasi afadhali kwa Magari madogo lakini sasa yanapita mpaka malori, barabara zimeanza kuharibika. Malori kuanzia sasa nisisikie yamekatisha ndani ya barabara za Mwendokasi.

"Lakini pia tutakwenda kufanya mapitio hii asilimia ya makusanyo ya mapato ya ndani inayopaswa kwenda kwenye barabara isiwe 10% ili muifanye TARURA iwe na uwezo wa kufanya kazi masaa 24 kusimamia ujenzi wa barabara katika maeneo yetu.
"Nendeni mkafungue barabara ambazo watu wanapaswa kupita kumaliza foleni, TARURA mkoa nendeni mkafikiri nini kifanyike ili mtengeneze barabara za kimkakati zinazoweza kupunguza foleni".

Mhe. Mchengerwa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Ujenzi wa Barabara kupitia DMDP zenye urefu wa kilomita 84.4.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news