Waziri Mhagama awasilisha ujumbe wa Rais Dkt.Samia kwa Rais wa Zambia

LUSAKA-Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Machi 25, 2025 amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Haikainde Hichielema katika Ikulu ya Rais iliyopo Jijini Lusaka Zambia.
Rais Hichielema amemshukuru Rais Samia kwa ujumbe huo maalum na kubainisha ya kuwa Zambia na Tanzania ni nchi zenye historia na ushirikiano wa kindugu muda mrefu na usio na mipaka.
Waziri Mhagama akiwa ameambatana na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule amemshukuru Rais Hichielema kwa mapokezi mazuri na ushirikiano imara ulipo baina ya Tanzania na Zambia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news