PWANI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua za maandalizi kuelekea sherehe za kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru ambao utazunguka katika Mikoa 31 na Halmashauri 195 nchini.


"Nimeridhishwa na maandalizi yaliyofanyika, mmefanya kazi kubwa hadi kufikia hatua hii, tuhakikishe sehemu ndogo zilizobaki tunazikamilisha kwa wakati."
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema maandalizi hayo yamefikia asilimia 96 na maeneo machache yaliyobaki yatakamilishwa ndani ya muda mfupi.
Awali, akitoa salamu za Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa huo Abubakar Kunenge amesema kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika kwa mafanikio makubwa.