LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 31, 2025 amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika sala ya Eid iliyofanyika kiwilaya kwenye Mtaa wa Maghalani, Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya sala hiyo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa waumini hao na Watanzania kwa ujumla kuliombea Taifa, viongozi wake pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano.