Waziri Mkuu azindua lango la utalii Hifadhi ya Mkomazi

KILIMANJARO-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyoko Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini.
Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa jipe, Faru weusi pamoja na tembo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news