Yanga SC yatoa msimamo kuahirishwa Kariakoo Derby, yataka vigogo watimuliwe Bodi ya Ligi Kuu

DAR-Kamati ya Utendaji wa Yanga SC katika kikao chake cha leo Machi 9, 2025 imetoa msimamo wake kuhusu uamuzi huo wa Bodi ya Ligi kuahirisha mechi yake na Simba SC tarehe 8 Machi,2025 huku ikitoa pole kwa wanachama, mashabiki,wapenzi na wadau wa mchezo wa mpira wa miguu waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani na kushindwa kushuhudia mechi hiyo.
Pia,Kamati ya Utendaji ya Yanga Sc imeitaka Bodi ya Ligi kuipa klabu hiyo haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi. Katika hatua nyingine Kamati ya Utendaji ya Yanga Sc imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote itakayopangwa.

Vilevile kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya Yanga imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo.

Hivyo klabu hiyo imeliomba Shirikisho la Mpira wa miguu (TFF) kuivunja kamati hiyo na kuteua viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news