ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Zanzibar inafanya kila juhudi kuhakikisha inaongeza idadi ya watalii kutoka barani Asia.
Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi Mosi,2025 alipozungumza na waigizaji na watengenezaji wa filamu kutoka India waliofika Ikulu Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar iko tayari kushirikiana na India kutangaza Vivutio vya Utalii nchini humo na kuwataka kuwa Mabalozi Wazuri watakapokuwa nchini kwao.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesema Uzoefu na Umahiri wa Waigizaji na Watengezaji wa Filamu wa India ni fursa Muhimu inayoweza kutumika kuitangaza Zanzibar ili Kuongeza Watalii kutoka India.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza kwa kuja nchini na Serikali ipo tayari kushirikiana nao kikamilifu kuitangaza Sekta ya Utalii ya Zanzibar.