KILIMANJARO-Watu nane wamefariki dunia na wengine 31 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Jeremiah Mkomagi amesema kuwa, tukio hilo limetokea Aprili 3,2025 majira ya asubuhi katika barabara ya Ugweno kwenda Mwanga.
Amesema kuwa, basi la Kampuni ya Mvungi lililokuwa likitokea Vuchama Ugweno kuelekea jiji Dar es salaam lilipokuwa likilikwepa gari dogo ndipo lilienda pembezoni mwa ngema ya mlima ambapo uzito uliizidi ngema na kupelekea kuanguka bondeni.
Kamanda huyo amesema,watu saba walifariki eneo la tukio na mmoja alifariki wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda ya KCMC na wengine 31 kujeruhiwa ambapo majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Kifula pamoja na Hospitali ya Kanda KCMC mkoani hapa.