MARA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia Sijali William Hence na Ilinus Mushumbusi ambao ni askari wa Jeshi la Magereza wanaohudumu katika Gereza la Tabora B Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Emmanuel Lucas (18) mkazi wa Kijiji cha Kisangura wilayani Serengeti.