Bado siku tatu kuelekea Kongamano la Kodi na Uwekezaji 2025
DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kodi na Uwekezaji 2025 litakalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.