ZANZIBAR-Bodi ya Ligi Kuu Zanzibar imesogeza mbele Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ Premier League) hadi Aprili 10, 2025 kutokana na kutokamilika kwa miundombinu katika viwanja vilivyopangwa kutumika kwa ajili ya ligi hiyo.
Ligi Kuu ya PBZ ilipangwa kurudi Aprili 05, 2025 baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ikipangwa kuchezwa katika Viwanja vya Mau A na Mau B kwa Unguja, na Gombani Stadium kwa upande wa Pemba.