BoT yatoa ufafanuzi wa Noti ya Shilingi 10,000 na 5,000 toleo la 2003 zinazoondolewa kwenye mzunguko

BENKI Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taharuki iliyojitokeza kuhusiana na noti za shilingi 10,000 na 5,000 toleo la 2003 zinazopaswa kuondolewa kwenye mzunguko zinazofananishwa na noti za thamani hiyo toleo la 2010 zinazoendelea kutumika.

Zoezi la kubadilisha noti hizo lilianza rasmi tarehe 06 Januari 2025 na litafikia ukomo tarehe 05 Aprili 2025 kama ilivyoainishwa kupitia tangazo la Serikali namba 857 na 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Noti hizo za mwaka 2003 ambazo zinaondolewa kwenye mzunguko na kukoma kutumika kuanzia tarehe 06 Aprili 2025 ni kama zinavyonekana hapa chini.

Noti za Shilingi 10,000 na 5,000 ambazo ni toleo la 2010 na marejeo yake zinaendelea kutumika na hivyo hazihusiki kwenye zoezi hili la ubadilishwaji linaloendelea;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news