CAIRO-Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rasmi rufaa iliyowasilishwa na Young Africans Sports Club dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba.
Ni kufuatia uamuzi uliotolewa na TPLB wa kuahirishwa kwa Kariakoo Derby iliyotakiwa kupigwa Machi 8,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
TFF, TPLB na Simba wamepewa siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea taarifa hiyo ili kuandaa na kuwasilisha utetezi wao na kesi hiyo itasikilizwa kwa haraka chini ya kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 huku pande zote zikitarajiwa kuwasilisha vielelezo na hoja zao.