Dkt.Kikwete atembelea makazi ya Mfalme Haile Selassie mjini Addis Ababa

ADDIS ABABA-Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametembea Qasir la Taifa la Ethiopia ambalo lilikuwa makazi ya Mfalme Haile Selassie.
Mhe. Kikwete alitembelea Qasir hilo kufuatia maombi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dkt. Abiy Ahmed ambapo walikutana jijini Addis Ababa Aprili 11, 2025 kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Qasir hilo ambalo kwa sasa limegeuzwa kuwa makumbusho ni eneo muhimu kwa kuwa limekusanya urithi wa utamaduni wa Ethiopia ambao kimsingi bado haujatumika ipasavyo kwa faida ya wananchi wa Taifa hilo.
Awali, Mhe. Kikwete alikutana na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wakiongozwa na Balozi Innocent Shiyo na kuwasihi kushikamana na utamaduni wa Tanzania ambao miaka yote umekuwa ukihamasisha umoja barani Afrika.

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post