WASHINGTON-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Sweden, Bi. Diana Janse kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe, ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia ya mwaka 2025, inayofanyika jijini Washington D.C nchini Marekani.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa Marekani, jijini Washington, Dkt. Mwamba na mgeni wake, wamejadiliana masuala kadhaa ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Sweden, ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali na pia kuendeleza mashirikiano ya kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.