Dkt.Natu El-Maamry Mwamba afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Climate Investment Funds (CIF)

WASHINGTON-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji katika Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Investment Funds (CIF), Bi. Tariye Gbadegesin, Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe, ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia ya mwaka 2025, inayofanyika jijini Washington D.C nchini Marekani.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Jijini Washington, Dkt. Mwamba na mgeni wake, wamejadiliana masuala kadhaa kuhusu jinsi Mfuko wa CIF unavyoweza kusaidia juhudi za Tanzania katika kutekeleza Mpango wa Nishati (Energy Compact) na kuendeleza vipaumbele vya matumizi ya Nishati safi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news