Dkt.Natu El-maamry Mwamba ateta na timu ya Benki ya Dunia

WASHINGTON-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Benki ya Dunia Tanzania, ikiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo hususan Utekelezaji wa miradi inayotekelezwa nchini, pamoja na miradi inayotarajiwa kufadhiliwa na Benki hiyo kupitia mzunguko wa IDA 21, tukio lililofanyika kando ya Mikutano ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, Katibu wa Baraza la Mawaziri, Bw. Nsubili Joshua na Mshauri wa Mhe. Rais, masuala ya uchumi, Dkt. Blandina Kilama, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news