WASHINGTON-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Fedha ya Kimataifa ya Benki ya Dunia (IFC), Bw. John Gandolfo, katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Tanzania, jijini Washington D.C., Marekani.

Gavana Tutuba alieleza kuwa uchumi wa Tanzania ni imara na thabiti, jambo linalodhihirishwa na viashiria mbalimbali vya kiuchumi.
Alitoa wito kwa IFC pamoja na mashirika mengine ya kimataifa kuwawezesha kifedha wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.