WASHINGTON-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, pamoja na Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, wameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika, uliofanyika katika Ofisi za Kamisheni ya Umoja wa Afrika, sambamba na mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), mjini Washington D.C., Marekani.

Aidha, mjadala katika mkutano huo uliangazia umuhimu wa Afrika kuwa na sauti moja katika kushawishi nchi za G20 kufanya mabadiliko yatakayorahisisha upatikanaji wa fedha na mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea.
Pia, walijadili namna ya kukabiliana na changamoto ya madeni, ambalo ni tatizo linalozikumba nchi nyingi za Afrika kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kijiografia, na kisiasa.