Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yatangaza nafasi za kazi

DODOMA-Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza nafasi za kazi za mratibu wa uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi na msimamizi msaidizi wa uchuguzi ngazi ya jimbo watakaosimamia Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara kwa upande wa Tanzania Zanzibar.
Kwa mujibu wa tangazo la Tume lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima, R. K, nafasi hizo ni kwa Unguja na Pemba na wanaotakiwa kuomba nafasi hizo ni raia wa Tanzania, watumishi wa umma na sifa nyingine zilizoainishwa kulingana na nafasi inayoombwa.

Tangazo hilo limemtaka kila mwaombaji aainishe nafasi anayoiomba, akitaja wilaya au jimbo analotaka kufanyia kazi na aambatishe vyeti vya elimu pamoja na maelezo binafsi (CV) na maombi yatapokelewa kuanzia tarehe 3 Aprili, 2025 hadi tarehe 23 Aprili, 2025 saa 9:30 Alasiri.

Maombi hayo yanatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara kwa upande wa Unguja na Chakechake (Mtaa wa Miembeni) kwa upande wa Pemba kwa anuani ya Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ofisi ya Zanzibar, Mtaa wa Maisara, S. L. P 4670, Zanzibar. SOMA ZAIDI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news