MWANZA-Mawasiliano ya Barabara kati ya Jiji la Mwanza na Mkoa wa Shinyanga yamekatika usiku wa kuamkia leo baada ya Daraja la Mkuyuni kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo hayo.
Daraja la Mkuyuni limekuwa likikumbwa na changamoto za muda mrefu, ambapo lilikuwa likifanyiwa ujenzi wa upanuzi na Serikali kupitia mkandarasi.
Aidha, ujenzi huo umecheleweshwa kwa muda mrefu, hali ambayo imeongeza usumbufu kwa wananchi na wasafiri.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Pascal Ambrose amesema,Serikali imetenga shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo ujenzi ulianza mwezi Januari,2025 na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Slisisitiza kuwa, licha ya changamoto zilizojitokeza, serikali inaendelea kuhakikisha kuwa mradi huu unakamilika kwa wakati.
Pia, amesema Serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa kazi inaendelea, na watafanya kila liwezekanalo ili daraja hilo likamilike kwa wakati.