Wizara yatoa ufafanuzi mama anayedai kubadilishiwa mtoto baada ya kujifungua

ARUSHA-Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya mkazi wa Daraja mbili mkoani Arusha Bi. Neema Kilugala aliyejifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, Mount Meru tarehe 24 Machi, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo April 2, 2025 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inaeleza kuwa, Bi. Neema anadai kuwa baada ya kujifungua alioneshwa mtoto wake na muuguzi akiwa ni mzima.

Hata hivyo, aligundua kuwa amebadilishiwa mtoto wake baada ya kuletewa mtoto akiwa amefungwa na vitenge ambavyo si vya kwake.

Muuguzi wa hosptali hiyo alidai kuwa alichanganya vitenge na vya mtoto mwingine hivyo akaahidi kwenda kubadilisha, pamoja na kuchukua hatua hiyo bado kulikuwa na hali ya sintofahamu.

Kufuatia hali hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha pamoja na Jeshi la Polisi imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuchukua sampuli za wazazi waliojifungua kipindi hicho pamoja na za watoto kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pia,kumsimamisha kazi muuguzi aliyemhudumia ili kupisha uchunguzi baada ya uchunguzi kukamilika taarifa rasmi zitatolewa na hatua stahiki zitachukuliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news