LUSAKA-Mashabiki wa Klabu ya Nkana wametuhumiwa kuvunja viti katika Dimba la Levy Mwanawasa baada ya Power Dynamos kupewa penalti kupitia Derby ya Kitwe.
Kutokana na changamoto hiyo kubwa ambayo inachangia kudhoofisha miundombinu ya soka kwa Zambia na barani Afrika,wananchi wameitaka Bodi ya Ligi Kuu ya Zambia kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa timu nyingine.
Inadaiwa mashabiki hao walichukua uamuzi huo baada ya kuwa na uhakika wa alama tatu ambazo zilitokana na bao lililofungwa na Jacob Ngulube dakika ya 80' katika michuano ya MTN Super League. Lakini, baada ya Power Dynamos kupewa penalti inayodaiwa yenye utata waliwalitibua mashabiki hao.Brian Masaninga wa Power Dynamos dakika ya 90+ kupitia penalti hiyo alisababisha ubao wa matokeo usome bao 1-1, hivyo kugawana alama moja kila mmoja.
■MTN Super League season 2024/25 week 32 standings