TANGA-Timu ya Kengold FC imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwenda Ligi ya Championship.
Ni kufuatia kipigo cha 2-1 dhidi ya Coastal Union katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
KenGold FC yenye alama 16 wakiwa mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa sasa wamesaliwa na mechi tatu ambapo hata wakishinda zote hawawezi kuifikia Tanzania Prisons waliopo nafasi ya 14 wakiwa na alama 27.
