Naibu Waziri Nderiananga afanya mazungumzo na Rais wa IFAD

BERLIN-Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Gérardine Mukeshimana, katika kikao cha pembezoni mwa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu uliofanyika tarehe 2–3 Aprili, 2025 mjini Berlin, Ujerumani.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ummy amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendeleza ushirikiano na IFAD katika kuimarisha miradi ya kilimo inayolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa maendeleo jumuishi.
Viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya maendeleo jumuishi ili kuhakikisha programu za kilimo zinakuwa shirikishi, zenye usawa, na zenye manufaa kwa jamii nzima.
Kupitia IFAD, Tanzania inaendelea kutekeleza Mradi wa Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) na Mradi wa Mageuzi ya Sekta ya Maziwa kwa Njia Endelevu ya Hali ya Hewa (C-SDTP), miradi inayochangia ustawi wa wananchi na kujenga mazingira jumuishi kwa watu wenye ulemavu katika sekta ya kilimo na mifugo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news