BERLIN-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Ummy Nderiananga ametembelea na kujionea shughuli zinazotekelezwa na taasisi mbalimbali kuhusu watu wenye ulemavu duniani wakati wa maonesho yanayoendelea katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa Watu wenye Ulemavu (Third Global Disability Summit) jijini Berlin nchini Ujerumani tarehe 03 Aprili 2025.