KAMPALA-Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu ameshiriki Mkutano wa 8 Kimataifa wa Jukwaa la Uongozi Africa (African Leadership Forum) unaoendelea kwa muda wa siku nne jijini Kampala nchini Uganda.

Pia,katika Mkutano huo Washiriki watapata fursa ya kujadili masuala muhimu kuhusu mustakabali wa Bara la Afrika katika nyanja za Elimu, Afya na pia juu ya suala mabadiliko ya Tabia Nchi.
Akizungumza katika mkutano huo, Mhe.Sangu amesema ili kutimiza malengo endelevu Barani Afrika (SDG's) kunahitajika mikakati maalum inayolingana na mazingira ya kila nchi.
Amesema, licha ya kuwepo kwa changamoto kubwa zinazolikumba bara la Afrika kwa ujumla kama vile mabadiliko ya tabia nchi, rushwa, idadi kubwa ya vijana wasio kuwa na ajira, na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi kwa nchi nyingi Barani Afrika.

Amesisitiza kuwa ili kukabiliana na hayo ni lazima kuimarisha ushirikiano wa kikanda kwa kuondoa vikwazo visivyokuwa vya lazima ili kuleta mabadiliko chanya ambayo yatapelekea kupunguza changamoto hizo na kufanikisha malengo haya kufikia mwaka 2030.
Mkutano huo, umehudhuriwa viongozi wandamizi kutoka nchi mbalimbali pamoja na Marais Wastaafu kutoka Bara la Afrika akiwemo Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dr. Jakaya Kikwete ambaye pia ni mlezi wa Jukwaa hilo la viongozi Barani Afrika , Rais Mstaafu Tunisia Mhe. Mohamed Marzouk, Rais Mstaafu wa Sierra Leone, Mhe. Ernest Koroma pamojq na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Boshe.